Thursday, July 31, 2014

KISUMO KWA KIKWETE: CHUNGA SANA UKAWA HUENDA WANA MTEGO

Peter Kisumo kulia akiwa na  Kingunge katikati na Fredrick Sumaye kushoto
Moshi. Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo amemtaka Rais Jakaya Kikwete na chama chake, CCM kuwa makini na msimamo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akisema haamini kama umoja huo umesema kila unachokusudia kukifanya.
Badala yake Kisumo alisema kinachofanywa na Ukawa ni mbinu za kujiimarisha kisiasa, jambo alilolisema iwapo CCM na Serikali yake haitakuwa makini, huenda ikaingia katika mtego na kushindwa kujinasua baada ya umoja huo kuimarika.
Kauli ya Mzee Kisumo imekuja wakati ambao viongozi wa Ukawa wameendelea kusisitiza kwamba wataendelea kususia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba vinavyoanza mjini Dodoma, Agosti 5 mwaka huu, hadi pale madai yao yatakapozingatiwa.

SAKATA LA IPTL JISOMEE MWENYEWE

Utata wa Serikali kwa IPTL
WAKATI Harbinder Sing Sethi, anadai alinunua asilimia 70 ya hisa za Mechmar kwa kiasi cha sh. milioni 500 ($300,000) ndani ya wiki tatu tu tangu hisa hizo kuuzwa kwa kampuni moja ya Visiwa vya Uingereza vya Virgin kwa sh. milioni sita tu, Tanzania Daima Jumatano limegundua uwepo wa utata.
Barua ya TRA Mkoa wa Ilala, iliyosainiwa na Meneja, Paschal Kabunduguru, yenye kumbukumbu nambari TRA/DR/ILA/RE/175 ya tarehe 15/11/2013, inaonyesha kuwa kampuni ya Mechmar ya Malaysia iliuza hisa zake asilimia 70 katika kampuni ya IPTL kwa kampuni ya Piper Links investment limited mnamo tarehe 9/9/2013 kwa thamani ya sh. 6,000,000.(milioni sita).

LOWASSA AMTUMIA ZITTO KUBOMOA CHADEMA?

                               
IMEGUNDULIKA kwamba Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) ndiye mfadhili mkuu na mpanga mikakati mkuu wa kundi linalomfuata Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambalo limeanzisha chama kipya cha siasa, Allaince for Change and Transparency (ACT-Tanzania).
Kwa wiki kadhaa za hivi karibuni, makundi ya wanachama, washauri na wapanga mikakati wa Lowassa na Zitto wamekuwa wakikutana katika maeneo kadhaa jijini Dar es Salaam na kupeana mbinu, lengo kuu likiwa ni jinsi ya kumega Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mapande ili kidhoofike kabla ya uchaguzi mkuu 2015.

Sunday, July 27, 2014

TUKUMBUSHANE:MAREHEMU MANDELA ENZI ZA UHAI WAKE AKIPOKEA BUTI ALIZOZIACHA NYUMBANI KWA MAREHEMU SWAI NSILOMBUNGE WA CCM ATAKA WANANCHI WABEBE SILAHA KUPINGA BOMOA BOMOA YA SERIKALI

Mbunge Malole (kulia) akionyeshwa mabaki ya nyumba ya kimila ya wagogo iliyobomolewa na CDA, anayemuonyesha  mabaki hayo ni mtemi wa kabila la wagogo mtemi Lazaro Chihoma
MBUNGE wa Dodoma Mjini, David Malole (CCM), amewahamasisha wananchi wa Kitongoji cha Mbuyuni, Kata ya Kizota, kununua silaha kwa ajili ya kuwazuia viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), watakaotekeleza bomoa bomoa.
Alisema kuwa ameamua kuwataka wananchi hao kujilinda wenyewe kutokana na serikali inayoongozwa na chama alichopo kushindwa kusimamia demokrasia na kufanya kazi kidikteta.

KUVURUGIKA KWA BUNGE LA KATIBA CHANZO NI SITTA,MIGIRO NA SULUHU?

      
MTETEZI wa haki za wanawake, Ananilea Nkya, amesema kuvurugika kwa Bunge Maalum la Katiba, wa kulaumiwa ni Mwenyekiti Samuel Sitta, Makamu wake Samia Suluhu na Waziri wa Katiba na Sheria, Asha Rose Migiro.
Akizungumza juzi katika kipindi cha ‘Kipima joto’ kinachorushwa na runinga ya ITV, Nkya, alisema kuwa hakuna sababu ya kumtafuta mchawi wa kushindwa kupatikana katiba mpya kwani viongozi hao ndio chanzo cha mparaganyiko.

DIWANI WA CHADEMA AHARIFU AMRI YA VIONGOZI WAKE NA KUIPIGIA DEBE CCM

Mbeya. Diwani wa Kata ya Masoko, Mbeya Vijijini kupitia Chadema, Edward Mwampamba , juzi alikiweka njiapanda chama chake baada ya kujitoa katika kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na kumsifia mgombea wa CCM kwamba anafaa kupewa kura zote.
Tukio lilitokea kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo na kuwafanya madiwai wa CCM kushangilia.

BUKUKU APATA AJALI DODOMA

Dodoma. Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Bahati Bukuku (40) amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongwa na gari aina ya Fuso wilayani Kongwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema ajali hiyo ilitokea alfajiri saa 9.00 jana katika barabara ya Morogoro Dodoma eneo la Ranch ya Narco.
Alisema ajali hiyo ilitokea baada ya gari walilokuwa wakisafiria yeye na mwimbaji mwingine wa Injili Frank Christopher (20), aina ya Toyota Nadia yenye namba za usajili IT 7945, kugongwa na Fuso na kuacha njia kisha kugonga gema.

MGULU AWAOMBA UKAWA KURUDI BUNGENI

Mwanza/Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM bara), Mwigulu Nchemba ameutaka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kurejea bungeni ili kukamilisha Mchakato wa Katiba Mpya kwa amani na utulivu.
Rai hiyo imekuja wakati mijadala mbalimbali inaendelea juu ya hatima ya wajumbe hao na mchakato huo tangu walipotoka bungeni na kususia vikao vya Bunge hilo Aprili 17 na kukataa kurejea, huku zikiwa zimesalia siku tisa kabla ya Bunge hilo kuendelea na vikao vyake mjini Dodoma Agosti 5.

BUNGE LA KATIBA: WATAALAMU WADAI SITTA HANA UWEZO WA KUREKEBISHA SHERIA

Dar es Salaam. Wakati Bunge Maalumu la Katiba linakusudia kufanyia marekebisho kanuni zake ili kuwabana wajumbe wa Bunge hilo ambao wamesusia kushiriki mchakato wa Katiba, wanasheria, wasomi na wanaharakati wamepinga dhamira hiyo wakisema itasababisha kuvunjwa kwa Katiba.
Wajumbe wanaolengwa katika marekebisho hayo ni wale wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutoka Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na baadhi ya wajumbe kutoka Kundi la 201 walioteuliwa na Rais.
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki alisema mabadiliko yanayokusudiwa kufanywa yatahusisha masuala ya nidhamu, yakiwamo fujo na utoro, mambo ambayo hivi sasa hayawezi kudhibitiwa moja kwa moja na mwenyekiti wa Bunge hilo.